




Aina hizi za Mashine ambazo hufahamika kama Dragon machines (Guns) zilianza kutengenezwa kuanzia miaka ya 60, zikiwa zimeboreshwa zaidi kuliko zile za Shrapnal. Hizi zina uwezo wa kutumia sindano zaidi ya moja na huja na sindano za kuchorea (outliners), za kuweka kivuli (shaders) na za kupaka (coloring). Pia umeme wake wake hufika mpaka volti 15. Michora hutoka bora zaidi kushinda ya Sharpnal. Bongo Ink kwa kuzingatia hali tofauti za uchumi nchini, tunatumia aina zote hizi 2 za mashine. Dragon Machines hutumiwa kwa wale wanaoweza kumuda gharama na wanaojali ubora zaidi. Mashine tunayotumia ni ya kimataifa na hutoa michoro yenye ubora wa kiwango cha juu. Karibuni sana
No comments:
Post a Comment